Ingia kwenye Mfumo

  • Utatakiwa kuwa na akaunti na nywila, kisha ingia kwenye mfumo.

Dodoso Jipya

  • Bofya kitufe kilichoandikwa "Surveys" kisha bofya "Create".

Taarifa za Dodoso Jipya

Taarifa zifuatazo ni muhimu.
  • Survey title: Hutumika kutambulisha Dodoso lako.
  • Base language: Lugha ya Msingi katika Dodoso. Kwa sasa mfumo unatumia kiingereza pekee
  • Description: Maelezo mafupi kuhusu Dodoso.
  • Welcome: Maelezo ya utambulisho wa Dodoso kwa washiriki. Hapa unaweza kueleza lengo,maana,utaratibu wa kujibu na taarifa nyinginezo
  • End message: Maelezo yatakayo kaa mwisho wa Dodoso baada ya maswali.
  • Baada ya kujaza taarifa za awali ni muhimu kuhufadhi. Bofya Save

Tengeneza Vipengele Vya Maswali

Baada ya kujaza taarifa za Dodoso, utaletwa kwenye ukurasa wenye mipangilio (settings) ya Dodoso. Ili kutengeneza maswali, bofya Structure
  • Title: Hapa utajaza jina la kipengele. mfano, PART A, SECTION A
  • Description: Maelezo juu ya Kipengele.
  • Baada ya kujaza taarifa bofya Save and add question

Tengeneza Maswali

  • Jaza taarifa zote kama zinavyo hitajika
  • Baada ya kujaza taarifa za swali bofya Save and add question, kwa swali lingine la kipengele hicho.

Weka Dodoso tayari kwa kujibiwa

Baada ya kujaza taarifa za Dodoso na kuandaa maswali, sasa unaweza kuliweka tayari kwa kujibiwa/kusambaza kwakubofya "Activate this Survey".
  • Unaweza kusambaza kwa kutuma kiunganishi (link) inayooneka kwenye sehemu ya "Share your survey"
  • Pia unaweza kusambaza kwa kutumia namba ya Dodoso (Survey ID) inayopatikana kwenye "Survey Summary"
    UNASHAURIWA KUSAMBAZA DODOSO LAKO KWA KUTUMIA NAMBA YA DODOSO BADALA YA KIUNGANISHI (link).